Kanuni na Masharti

             
1. Mawanda na Matumizi
Kanuni na masharti haya yanaunda mkataba kati ya Mteja na Benki.  Mteja ataomba kwa Benki kwa kutumia fomu iliyotolewa kwa kuendesha Akaunti na kutumia huduma zinazohusiana.  Kwa kuomba kufungua Akaunti, Mteja anatakiwa kusoma, kuelewa na kukubali kanuni na masharti haya.  Kwa nyongeza, Kanuni na masharti mahususi yoyote yanayohusika na ada zilizowekwa katika Mwongozo wa Ushuru vitatumika.  Katika hali ya mwingiliano wowote kati ya Kanuni na Masharti na Kanuni Mahususi na zinazohusiana na bidhaa maalumu yoyote au akaunti, Kanuni na Masharti Mahuhusi yanayohusika vitatumika.

2. Fasili
Katika kanuni na masharti haya, maneno na kauli zitakuwa na maana zilizoelezwa hapa chini isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. 
“Akaunti” ina maana akaunti iliyofunguliwa na kuendelezwa na kwa mujibu wa maelezo ya upande wa pili na Akaunti nyingine yoyote iliyofunguliwa na Mteja kwenye Benki ya National Microfinance PLC.
“ATM” ina maana Mashine Inayojiendesha Yenyewe
“Benki” ina maana National Microfinance Bank PLC ikiwa na ofisi yake ya usajili
Dar es Salaam pamoja na matawi mbalimbali Tanzania nzima.
“Kadi” Ina maana Kadi ya Elektroni ya Kutolea fedha inayotolewa na Benki kwa maombi na kwa jina la mtu aliyeandikwa kwenye kadi kwa matumizi yanayohusiana na huduma za kadi ya kutolea fedha zinazotolewa.
“Mwenyekadi” ina maana mtu ambaye kadi yake inapaswa kutolewa fedha kulingana na kumbukumbu za kadi na kwa yule aliyepewa Kadi.  Majina yao pia yanaandikwa kwenye Kadi na wanakubali kufuata kanuni na mashati kama yatakavyobadilika mara kwa mara.
“Mteja” ina maana mtu yeyote mwenye Akaunti Benki.
“Huduma” ina maana huduma zinazotolewa na Benki zinazohusiana na Akaunti na hasa zaidi zilizoelezwa katika masharti haya.
“PIN” ina maana Namba ya Utambulisho Binafsi inayochaguliwa na Mwenye Kadi kwa ajili ya matumizi ya kadi yake.

3. Ufafanuzi
a. Marejeo yote yaliyo katika umoja yanajumuisha wingi na vivyo hivyo  kinyume chake na neno “Kujumuisha” linapaswa kutafsiriwa kama “bila ya kikomo”.
b. Neno linalomaanisha jinsia yoyote linajumuisha jinsia nyingine.
c. Marejeo kwa sheria yoyote ya kampuni, sheria au sheria nyingine yanajumuisha kanuni zote na hati nyingine na uunganishaji wote, marekebisho, utungaji upya au ubadilishaji wa sheria kwa wakati inapokuwa katika utekelezaji.
d. Vichwa vya habari vyote, uchapaji kwa herufi nzito na italiki (kama upo) vimeingizwa kwa ajili ya kurahisisha marejeo.

4. Marekebisho ya Kanuni na Masharti
Benki itakuwa na uamuzi wa mwisho wa kurekebisha au kuongeza Kanuni na Masharti na Kanuni na Masharti yoyote Mahususi (ikiwa ni pamoja na viwango vya riba na gharama zozote za Benki) wakati wowote. Mteja atafahamishwa kuhusiana na mabadiliko yoyote kwa namna itakayoamuliwa na benki.

5. Kufungua Akaunti; Kumbukumbu za Kutoa
5.1 Ili kufungua akaunti Benki, waombaji lazima (i) wajaze fomu inayohusika ya maombi inayotolewa na benki ili kuwe na majibu sahihi na ya kina kwa maswali yote yanayoulizwa na Benki; (ii) waambatishe nyaraka zote zilizotajwa katika fomu hiyo ya maombi; na (iii) watoe taarifa nyingine zote kama hizo au nyaraka zitakazoombwa na benki.
5.2 Mwombaji lazima athibitishwe na mtu wa tatu anayeaminika, ambaye utambulisho wake utakubaliwa na Benki kabla, na Benki ina haki ya kutafuta na kuchukua kumbukumbu kwa waombaji hao.
5.3 Benki, inapopokea maombi ya kufungua akaunti na baada ya hapo wakati wowote, inaweza kuuliza kuhusu kumbukumbu za mkopo wa mteja na mashirika ya mkopo au watu wengine kama Benki itaona ni muhimu au inafaa.
5.4 Ni pale tu benki itakapothibitisha kwa mteja kuhusu mafanikio ya utambulisho wake na kurekodi data zake Benki itafungua Akaunti kwa ajili ya Mteja.
5.5 Pale Mteja atakapotoa maombi ya maandishi kwa Benki, Benki inaweza (lakini haitalazimika) kutoa taarifa kwa mashirika ya mikopo na benki nyingine kwa kuzingatia uendeshaji wa akaunti yoyote ya Mteja kwa Benki hataingia deni kwa kufanya hivyo.

6. Watia saini walioidhinishwa
Mteja atatoa sampuli ya saini za Wateja na maelezo ya watia saini walioidhinishwa (na atahakikisha kwamba mtia saini yeyote aliyeidhinishwa anatoa sampuli ya saini), kama na wakati atakapohitajiwa kufanya hivyo na Benki.

7. Utunzaji salama
Mteja pekee atawajibika na utunzaji salama na usiri wa taarifa za akaunti, cheti cha taarifa ya salio, kadi, PIN na vitu vingine kama hivyo vinavyohusiana na kufungamana na Akaunti.

 

8. Uendeshaji wa Akaunti
a. Miamala kwa kawaida hufanywa wakati wa saa za benki katika tawi ambapo Akaunti inatunzwa au katika matawi yoyote ya Benki.  Benki haitawajibika na uchelewaji wowote katika akaunti yoyote kwa kushindwa kuunganishwa.
b. Benki kwa uamuzi wake pekee inaweza kuzuia idadi ya utoaji fedha katika Akaunti.

9. Kutoa maelekezo
9.1 Benki itashughulikiwa maelekezo yaliyotolewa katika hati yenye saini halisi ya Mteja (au mtia saini wake aliyeidhinishwa).
9.2 Benki kwa uamuzi wake, katika mazingira fulani, inaweza kuruhusu maelekezo yatolewe kwa njia ya simu, baruapepe, nakala halisi au njia nyingine ili mradi taratibu za usalama za Benki zinazofaa zimefuatwa.
9.3 Benki inaweza kukataa kushughulikia maelekezo yoyote kama malekezo hayo yatakuwa hayaeleweki, au kama Benki inaamini kwamba: (i) kufanya hivyo kutaingilia sheria au kanuni yoyote inayotumika au; (ii) Benki kwa nia njema inaamini kwamba maelekezo yanaweza kuhusisha udanganyifu au mwenendo wowote mbaya wa uhalifu.

10. Wamiliki wa Akaunti ya pamoja
10.1 Pale ambapo akaunti itafunguliwa au kuendeshwa kwa jina la zaidi ya mtu mmoja, haki na wajibu wa kila mmiliki wa akaunti ya pamoja na mambo mengine kutegemeana na uendeshaji wa akaunti yatakuwa kama ilivyokubaliwa kwa maandishi na kila mmoja wao na Benki mara kwa mara.
10.2 Kama hakutakuwapo makubalinao yaliyo kinyume na Kifungu 10.1, wamiliki wa akaunti watakuwa na dhima ya pamoja au baadhi, na kila mmiliki wa akaunti ya pamoja atachukuliwa kuwa na mamlaka kamili ya kuendesha akaunti, kutoa na kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya pamoja bila ya ridhaa ya wamiliki wengine wa akaunti.
10.3 Marejeo ya “Mteja” katika Kanuni na Masharti haya yatajumuisha kila mmiliki wa akaunti ya pamoja.

11. Akaunti Isiyotumika
11.1 Benki inaweza kuainisha Akaunti kama Isiyotumika endapo hakuna mteja anayeitumia akaunti kwa miezi 12.  Mteja kutumia akaunti itamaanisha kuingiza kokote fedha na kutoa kunakofanywa na Mteja katika akaunti yake kupitia njia zifuatazo:
I.   Kuweka / kutoa fedha
II.  Kutoa fedha kupitia ATM.
11.2 Benki kwa uamuzi wake pekee inaweza kuzuia Huduma na/au shughuli katika Akaunti ya mteja ambayo imeainishwa kama isiyotumika.

12. Mabadiliko ya Maelezo ya Mteja
Mteja anapaswa kuiarifu Benki mara moja kwa Maandishi (au, kwa uamuzi wa Benki au, njia nyingine yoyote) kuhusu mabadiliko yoyote ya jina au makazi au anwani ya mawasiliano (katika kila namna akitoa ushahidi kama Benki itakavyohitaji) au ufutaji wowote au mabadiliko katika uidhinishaji wowote unaofanywa na mteja huyo.
13. Huduma ya Uchukuaji
a. Hundi, hawala, bili, gawio/riba na hati nyingine zinazotolewa kwa maslahi ya Mteja zinakubaliwa kuchukuliwa kwa niaba ya Mteja.  Uchukuaji wa hati nje ya tawi unaingiza gharama za uchukuaji.  Benki haikubali jukumu lolote la upotevu, ucheleweshaji, uondoaji maneno au uzuiaji wa hati katika posta au kwa mtu anayepeleka barua.  Benki haikubali wala kushirikiana jukumu lolote kwa uchelewaji wa kupata hati hizo au kwa uhalisia, uhalali au usahihi wa saini au uidhinishaji uliomo.  Utoaji fedha kwa kutumia hati hizo unaruhusiwa tu kwa kutambuliwa kwa utaratibu na Benki.
b. Benki ina mamlaka ya kutoa fedha kwenye akaunti ili kulipia kiasi chochote kilichotolewa kimakosa kwenye Akaunti ya Mteja.
c. Hundi za nchini n.k. zinaweza kutangazwa kuchukuliwa mapema katika siku kama itakavyotakiwa kulingana na muda wa kawaida wa Benki Kuu.  Utoaji wa fedha kwa kutumia hundi zilizopitishwa kwa kawaida utaruhusiwa tu kupitia salio lililothibitishwa na Benki Kuu.
d. Endapo hundi itarejeshwa, kiasi ambacho kimeshaingizwa kwenye Akaunti ya Mteja na/au kuhusiana na utoaji fedha ulioruhusiwa, Benki itabatilisha uingizaji wa kiasi hicho na kukata kiasi kinacholingana na kiasi kilicho katika hundi iliyorejeshwa.
Kwa matukio kama hayo, kama Akaunti haitakuwa na fedha za kutosha, kiasi kilichobakia kitachukuliwa kuwa deni la muda linalodaiwa kwa Mteja na Mteja atalazimika kulipa kiasi hicho haraka atakapotakiwa na Benki kufanya hivyo.  Katika kukata kiasi hicho kama ilivyokwishasemwa, Benki itakata kiasi kinachodaiwa.  Gharama za huduma, adhabu na gharama nyinginezo kama zinavyotumika zitatozwa na Benki kwa namna hiyo.

14. Kifo au Kutojiweza
Mteja anakubali kuiarifu benki kwa haraka kama yeyote kati ya mmiliki wa pamoja wa akaunti au mtia saini aliyeidhinishwa katika Akaunti amefariki au mahakama imetamka kuwa hajiwezi.  Benki inaweza kusitisha Akaunti na kusimamisha shughuli zote pale ambapo yeyote kati ya wamiliki wa akaunti ya pamoja au watia saini walioidhinishwa watafariki au kutajwa kuwa hawawezi.  Benki inaweza kuendeleza usitishaji wa Akaunti hadi itakapopata utambulisho na hati za utambulisho wa warithi/ wanufaika kwa kuridhika kwake.

15. Kutohamishika
Akaunti na huduma zinazotolewa kwa Mteja hazihamishiki katika mazingira yoyote na zitatumiwa na Mteja tu.  Hata hivyo, Benki itakuwa na haki ya kuhamisha, kutoa au kuuza haki zake zote, marupurupu au wajibu kwa yeyote na Masharti haya yataendelea kutumika kwa manufaa ya warithi na kazi za Benki.

16. Taarifa
Taarifa zinazohusiana na Akaunti, huduma na shughuli nyingine zinazohusiana na Akaunti zinaweza kutolewa na Benki ama kwenye tawi au kwa kutuma barua kwenye anwani ya Mteja.  Taarifa zote kuhusiana na huduma au Akaunti zinazotolewa na Mteja kwa Benki zitakuwa kwa maandishi na kupelekwa kwenye tawi la Benki ambako Mteja alifungua Akaunti na taarifa zote zitachukuliwa kuwa zimepokewa na Benki baada tu ya kukubali kupokelewa kwa maandishi na Benki.

17. Miamala kupitia Elektroni
Benki inaweza kutoa huduma za ATM, taarifa kupitia ujumbe wa simu, huduma za Benki jongezi na Huduma za Benki katika Intaneti kwa Mteja.  Mteja atakubali kufuata na kukubaliana na kanuni na masharti yote hayo kama Benki itakavyoeleza mara kwa mara, na hapa anakubali na kuthibitisha kuwa miamala yote inayofanywa kwa njia ya elektroni, kompyuta, mtandao wa mashine inayojiendesha au kupitia njia nyingine za mawasiliano ya simu, zilizoanzishwa na au kwa niaba ya Benki, kwa ajili na kuhusiana na Akaunti, au bidhaa na huduma nyingine za Benki, zitaunda kisheria masharti na uhalali wa miamala inapofanywa kwa kufuata na kwa kutekeleza kanuni na masharti ya Benki kwa huduma hizo, kama itakavyoelezwa mara kwa mara.

18. Ubadilishaji Fedha
18.1 Benki itafanya miamala ya ubadilishaji fedha kwa mujibu wa kiwango kinachotumika Benki mara kwa mara.
18.2 Kiwango cha kubadilisha kinachotumika, isipokuwa kama kitakuwa kinakubaliwa na Mteja, kitazingatia kiwango kinachotumiwa na Benki kwa miamala kama hiyo wakati shughuli ya ubadilishaji fedha inapofanyika.

19. Ukopaji wa Mteja
19.1 Mteja ataweza kukopa fedha kutoka Benki pale tu masharti yaliyokubaliwa kwa maandishi kati ya Mteja na Benki yatazingatiwa.
19.2 Huduma yoyote kama hiyo lazima iidhinishwe kwanza na Benki katika kila tukio.  Mwombaji anakubali kwamba masharti ya huduma yoyote au ufadhili vinaweza kutolewa au kukataliwa kwa uamuzi pekee wa Benki.
19.3 Benki itatoza riba katika deni lolote katika akiba au huduma nyingine za kibenki, mchanganyiko au moja kama itakavyoamuliwa katika uamuzi pekee wa Benki (au kama itakavyokubaliwa kipekee kwa maandishi na Mteja).  Mteja anakubali bila kubadilisha na bila masharti kulipa riba yoyote au yote kwa Benki kama na wakati na kwa njia yoyote Benki inavyoamua au kuagiza.
19.4 Wateja watawajibika kwa kiasi chochote wanachodaiwa na Benki.

20. Malipo ya Riba
Riba inalipwa katika kiwango kinachozidi salio la chini la mkopo kinachoendelezwa katika kipindi fulani kitakachoamuliwa na benki.

21. Gharama, Ada na Matumizi; Makato kutoka kwenye Akaunti
21.1 Benki itakuwa na haki ya kutoza ada ya matumizi kama ilivyoelezwa katika Mwongozo wa Ushuru, kila ada itatofautiana mara kwa mara.
21.2 Benki itakuwa na haki (bila ya kuwasiliana na Mteja) kutoa fedha katika Akaunti yoyote ya Mteja kuhusiana na ada yoyote, matumizi (ikijumuisha, bila ya kikomo, gharama za sheria, kodi na ushuru wa stempu), riba, kamisheni zinazolipwa au zinatotumika kwa niaba yake, au gharama zinazotozwa kama matokeo ya shughuli yoyote kati ya Benki na Mteja.

22. Umiliki  Uanzishaji wa Benki
22.1 Kwa kuongezea umiliki wowote wa jumla au haki nyingine au marekebisho ambayo Benki inaweza kustahili iwe kwa uendeshaji wa sheria au vinginevyo, Benki, wakati wowote, na bila ya taarifa inaweza kuunganisha au kuweka pamoja akaunti yoyote au akaunti zote za mteja katika fedha yoyote au kuweka au kuhamisha kiasi chochote kilichobakia katika mkopo wa akaunti yoyote katika kulipia madeni yoyote ya Mteja kwa Benki yanayohusiana na akaunti nyingine yoyote au yanayohusiana na jambo jingine lolote, bila ya kujali kama madeni hayo ni mengi au ya pamoja.
22.2 Benki itakuwa na umiliki katika madai yote ambayo Mteja anastahili au ambayo Mteja atastahili yanayotokana na uhusiano kati ya Benki na Mteja.
22.3 Umiliki utakuwa kama dhamana kwa madai yote yaliyopo, ya baadaye na masharti dhidi ya Mteja, ambapo Benki inastahili kutokana na uhusiano wa shughuli za kibenki.

23. Kuvunja Uhusiano
23.1 Wakati wowote na bila ya kutoa sababu yoyote kwa taarifa ya maandishi, mteja anaweza kuvunja ama uhusiano wote na Benki au huduma maalumu zinazohusiana na bidhaa maalumu (kwa suala la umiliki wa pamoja, wamiliki wote wa akaunti lazima watie saini), uvunjaji huo usiwe na athari kwa haki zozote zinazotokana na kipindi cha kuvunja.
23.2 Wakati wowote na bila ya kutoa sababu yoyote baada ya kutoa taarifa ya maandishi ya siku 30 ya kuvunja uhusiano wote na Benki au Mteja au huduma nyingine maalumu, uvunjaji huo usiwe na athari kwa haki zozote zinazokuwapo katika kipindi cha uvunjaji. 
Hata hivyo, Benki itastahili kuvunja uhusiano wote na Mteja mara moja kama inaamini vya
kutosha kwamba (i) Mteja amekuwa akijihusisha katika udanganyifu au tabia nyingine za uhalifu; (ii) kuna Masharti ya Kanuni na Masharti au Kanuni na Masharti yoyote mahsusi ambayo yamevunjwa; (iii) Uhusiano kati ya Benki na Mteja umevunjika; au (iv) Mteja (ikiwa ni pamoja na mmiliki yeyote wa akaunti ya pamoja anayeunda sehemu ya Mteja) ameamuliwa kufilisiwa, amefilisika au masuala yao yamekuwa ya kiutawala, usimamizi au mchakato mwingine unaofanana na huu.
23.3 Kwenye ufungaji wa akaunti yoyote, Mteja atarejesha vitu kama ambavyo atatakiwa na benki hii (ikiwa ni pamoja na, bila kikomo, kadi zote na hundi ambazo hazijatumiwa).  Mteja mara moja atalipa tena kiasi chochote kilichosalia kwa ajili ya benki hii.

24 Dhima
24.1 Katika kanuni na masharti haya, uondoaji au uzuiaji wa dhima au marekebisho yatafaa tu kwa kiasi kwamba dhima au marekebisho:
24.1.1 Hayatokani na kifo au madhara ya 
mtu binafsi.
24.1.2 Yanaweza kisheria kuondolewa au kuwa na ukomo, na
24.1.3 Hayatokani na udanganyifu au ukosaji wa uaminifu wa mtu huyo anayehusika na uondolewaji au uzuiaji.
24.2 Si benki, maofisa wake, mawakala au waajiriwa watawajibika kwa utoaji usioidhinishwa kutoka au ufikiaji wa akaunti yoyote isipokuwa ambapo taarifa ya awali ya upotevu wa taarifa yoyote, fomu ya kutolea fedha au rekodi ya akaunti nyingine itatolewa kwa benki na kuthibitishwa kwa maandishi.
24.3 Ushahidi wowote wa maandishi utakaotolewa na benki kuhusiana na Akaunti ya Mteja utachukuliwa kuwa ndio wa mwisho na ushahidi wa kuthibitisha hali ya Akaunti ya Mteja.
24.4 Benki haitawajibika kwa Mteja kwa kushindwa kokote kutimiza masharti yoyote yanayosababishwa na hali zozote nje ya udhibiti wake mzuri au kwa kushindwa kutenda kulingana na Ibara ya 9.3
24.5 Dhima ya benki kwa Mteja kwa hasara au madhara yanayotokana na kushindwa, kuchelewa au kosa katika kufuata maelekezo katika tukio lolote utawekewa kikomo kwenye kiasi cha chini cha hasara au madhara hayo na kiasi cha faida yoyote ambayo haikupokelewa au kulipwa na Mteja kutokana na kushindwa huko, uchelewaji au kosa.  Benki haitawajibika kwa Mteja kwa hasara ya biashara, upotevu wa imani, upotevu wa fursa, upotevu wafaida au aina yoyote nyingine ya hasara maalumu, inayoandamana au ya moja kwa moja.
24.6 Benki haitawajibika kwa hasara zozote ambazo mteja ameingia kwa njia isiyo ya moja kwa moja au ambazo benki isingeweza kuzitabiri.
24.7 Benki haitawajibika kwa mteja kuhusiana na uchukuaji wa hatua yoyote inayotakiwa kisheria, ikiwa ni pamoja na, bila ukomo, kufuata agizo lolote la kuzuia  akaunti ya mteja au agizo lolote la jaji la uzuiaji wa akaunti ya mteja kutolipa pesa kwa mwia/ mdai 1 mpaka kwa amri ya mahakama.

25 Hati ya kusamehe madai
Hakuna kushindwa au kuchelewa kwa benki katika utekelezaji wa haki yoyote, uwezo/madaraka au marupurupu ambayo yametajwa hapa yataendeshwa kama hati ya kusamehe madai katika jambo pekee au kama sehemu ya haki nyingine, madaraka au marupurupu.  Haki na marekebisho ya Benki kama yalivyoelezwa hapa yatakuwa ya kulimbikiza na siyo pekee kwa haki zozote au marekebisho yaliyotolewa kisheria.

26 Fidia
a) Mteja hapa anakubali kwamba, yeye mteja kwa gharama zake mwenyewe atafidia, kulinda na kusimamia benki isiingie  hasara kutokana na au dhidi ya dhima zote, hasara nyingine yoyote ambayo inaweza kutokea, kutokana na au inayohusiana na uendeshaji au utumiaji wa akaunti hii au huduma hizi au, kuvunja, kutotenda au utendaji usiotosheleza wa mteja kwa mojawapo ya Kanuni na Sheria hizi, au vitendo hivi, makosa, mawasilisho, kutoelewa vema, mwenendo mbaya au uzembe wa mteja katika utekelezaji wa majukumu yake.
b) Benki kwa hali yoyote ile, haitawajibika kwa Mteja kwa hasara yoyote isiyo ya moja kwa moja, ya dharura, itakayosababishwa na madhara maalumu yanayohusiana na akaunti hii au huduma hizi.
c) Benki haitawajibika kwa kushindwa kokote kutekeleza jukumu lolote lililomo katika Masharti haya au kwa hasara yoyote au madhara yoyote yawayo yaliyosababishwa na mteja kwa hali yoyote ile  na iwe hasara hii au madhara haya yawe yanayodhaniwa kuwa ndiyo sababu (ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja) kwa mgogoro wowote au suala lingile lolote au hali yoyote.
d) Mteja atailipa fidia benki kama mlipaji wa hundi au hati za fedha kwa hasara yoyote au madhara ambayo benki inaweza kuingia kwa kudhamini uidhinishaji wowote au ulipaji  wa hundi, bili au hati nyingine zilizowasilishwa kwa ajili ya malipo na udhamini huu kama unavyotolewa na benki utachukuliwa kuwa umetolewa katika kila tukio kwa maombi ya haraka ya gharama za mteja.
e) Mteja ataifanya Benki ifidiwe kwa wakati wote dhidi ya, na kuiepusha benki kutopata madhara kutokana na vitendo vyote, mashauri, malalamiko, hasara, madhara, gharama, faida (kabla na baada ya hukumu kwa pamoja) na gharama zikijumuisha gharama za kisheria kwa vigezo vya gharama za mwanasheria na mteja) ambazo zinaweza kuletwa dhidi ya au kuingiwa na Benki katika kutatua mgogoro wowote kwenye Akaunti ya Mteja na Benki au katika utekelezaji wa haki za Benki au kuhusiana na Kanuni na Sheria hizi zilizopo katika jambo hili, au ambazo zinaweza kutokea moja kwa moja kwa au kwa njia isiyo ya moja kwa moja nje ya au kuhusiana na benki katika utekelezaji wa majukumu yake haya au kupokea maelekezo, ikiwa ni pamoja na, lakini yasiyokomea kwenye, fakisi na mawasiliano mengine ya simu au maelekezo ya kieletroni na kuyafanyia kazi au kushindwa kutekeleza.
f) Iwapo mteja anadaiwa kiasi chochote cha fedha na hajalipa kwa tarehe ipasayo, ikijumuisha bila ukomo fedha zozote zinazodaiwa chini ya aya hii, mteja huyu atawajibika kulipa riba ya kiasi hicho cha pesa ambacho hakijalipwa kwa kiwango au viwango vitakavyotolewa na Benki  mara kwa mara kutoka tarehe ambayo malipo hayo yalikuwa yanatakiwa kufanywa hadi tarehe ya malipo.
g) Mteja peke yake atawajibika katika kuhakikisha kwamba anafuata kikamilifu sheria na kanuni zozote zinazotumika katika utekelezaji wa sheria yoyote inayohusika na ufunguaji wa Akaunti yake katika Benki na ataifidia na kuhakikisha ufidiwaji wa Benki kutokana na vitendo vyote, mashauri, malalamiko, hasara, uharibifu, gharama (ikiwa ni pamoja na gharama za kisheria) ambazo zinaweza kuingiwa dhidi ya au kugharimiwa na Benki kutokana na kushindwa kokote kufuata Sheria au Kanuni yoyote ile.
h) Fidia kama ilivyotajwa itaendelea bila kujali ufungaji wa akaunti hii.

27 Udhibiti wa Data
Benki itapewa haki ya kutunza taarifa binafsi zilizotolewa na mteja na taarifa nyingine kuhusiana na au zinazohusu uhusiano kati ya Benki na Mteja kwenye kanzi data za kieletroni, mfumo wa kawaida wa kuingiza kwenye faili au kwa njia nyingine yoyote.  Tawi lolote la Benki ambalo mmiliki wa akaunti ana uhusiano linaweza kutumia na kusahihisha taarifa zozote muhimu zilizohifadhiwa ili kutoa huduma kwa mteja, kuepusha udanganyifu na kutengeneza upya rekodi zao binafsi kuhusu mteja.

28 Usiri
Benki itaendeleza na kulinda jukumu lake la usiri kuhusiana na masuala ya fedha ya Mteja kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania na sheria za huduma za Benki zinazokubalika Kimataifa. 
Benki itatoa tu taarifa zinazohusiana na akaunti ya mteja kama ina jukumu (au inatakiwa kisheria) kufanya hivyo, au kama mteja ataomba au atatoa idhini ya utoaji wa taarifa hiyo, ama kulingana na ibara ya 5.5 au vinginevyo.

29 Mawasiliano
29.1 Mpaka Benki iwe imetoa taarifa ya anuani maalumu kwa mteja, barua yoyote, notisi au hati nyingine inayohusiana na akaunti itaweza tu kuhifadhiwa kwenye benki na mteja kwenye tawi la benki ambako kimsingi mteja hufanyia biashara.
29.2  Benki inaweza kumpa mteja taarifa ya aina yoyote kwa namna ambayo benki  itaiona mahsusi. Barua yoyote, notisi au hati nyingine zilizohifadhiwa na benki kwa mteja zitachukuliwa kuwa zimehifadiwa, kama  zitapelekwa kwa njia ya posta na kutumwa kwa mteja kwa anuani waliyojulishwa kwa mara ya mwisho, saa 72 baada ya kuituma nchini Tanzania, na saa 144 kwa nchi nyingine yoyote.
29.3 Benki inaweza kufuatilia na kurekodi simu zilizopigwa kuhakikisha kwamba maelekezo ya mteja yamefanyika kwa usahihi na kuboresha ubora wa huduma za benki.
29.4 Benki inaweza kuwasiliana na mteja kuhusu huduma nyingine za benki ambazo Benki inaamini kwamba zinaweza kuwa za manufaa kwa mteja labda ikiwa mteja ataitaarifu Benki kwa maandishi kwamba hapendi kupokea taarifa hizo.
29.5 Mteja bila kukawia ataijulisha Benki kuhusu utokeaji wa tukio lolote ambalo litaifanya Benki kuvunja sehemu ya uhusiano wake au uhusiano wote na mteja kulingana na Ibara ya 23.2.

30 Hakuna Kizuizi
Mteja hataanzisha au kuruhusu kujikimu, fidia yoyote ya mali au maslahi ya mtu wa tatu kuhusu au dhidi ya akaunti yoyote ya Benki au fedha zozote katika jambo hili bila Benki kutoa idhini kabla, kwa njia ya maandishi.

31 Uhalali wa Kanuni na Masharti
Ikiwa sharti lolote katika Kanuni na Masharti haya au Kanuni na Masharti yoyote muhimu yanayohusika yameonekana kutokuwa thabiti, sharti hilo au sehemu ya sharti hilo itachukuliwa kuwa si sehemu ya Kanuni na Masharti haya au Kanuni na Masharti mahsusi kama itakavyoonekana inafaa.  Utekelezaji wa masharti yaliyobakia hautaathiriwa.

 

32 Matumizi ya Kadi
32.1 NMB itatoa kadi kwa Wateja ambao maombi yao yamekubalika.  Kadi zinapaswa kutumiwa na mmiliki wa kadi hii nchini Tanzania.
32.2 Kadi itabakia kuwa mali ya Benki na kuhusiana na ubatilisho ni lazima irejeshwe idaiwapo na Benki.
32.3 Kadi itamwezesha mmiliki wa kadi:
a) Kutoa fedha taslimu kutoka ATM yoyote ya NMB kwa shilingi za Kitanzania.
b) Kubadilisha Namba ya siri kwenye ATM zozote za NMB au kwenye matawi ya NMB.
c) Kupata salio la akaunti na taarifa fupi za miamala 10 ya mwisho.
d) Kuendesha huduma nyingine zozote za kadi ambazo zinaweza kutolewa na Benki siku hadi siku.

32.4 Utoaji wowote wa fedha kwenye ATM za NMB utategemea ukomo wa kutoa kila siku.
32.5 Kadi haitampa haitamwezesha mmiliki wa kadi kuzidi ukomo wa akaunti au kutoa  zaidi akaunti.
32.6 Rekodi za Benki kwa muamala wowote au matokeo yake katika hilo utakuwa wa kuthibitisha.
32.7 Matumizi yasiyo sahihi ya ATM au ya kuingiza kwa makosa namba ya siri yatasababisha uzuiaji kiautomatiki wa kadi hii, ambayo inaweza kurejeshwa kwa kwenda kwenye tawi la mteja pamoja na utambulisho sahihi.
32.8 NMB imeidhinishwa kutoa fedha kwenye akaunti ya mmiliki wa kadi kwa kiasi chote kitakachotolewa kwa njia ya kadi na namba ya siri.
32.9 Mmiliki wa kadi atalazimika kuchukua tahadhari zote kuhakikisha usalama wa kadi hii na usiri na namba ya siri wakati wote na kuepusha hasara ya au matumizi ya namba ya siri na mtu wa tatu.  Wamiliki wa akaunti ya pamoja watawajibika kikamilifu katika kuhakikisha kwamba namba ya siri inajulikana tu wakati wote kwa watu walioidhinishwa ambao wanamiliki akaunti ya pamoja.  Mmiliki wa kadi atawajibika kulingana na muamala wowote utakaofanywa kabla ya NMB kupokea taarifa ya hasara au wizi huo.
32.10 Kama kadi itapotea au kuibiwa, mmiliki wa kadi atalazimika kuijulisha Benki mara moja juu ya hasara hiyo au wizi kwa maandishi au kwa njia ya simu.
32.11 Wamiliki wa akaunti na wamiliki wa kadi watabakia pamoja na mbalimbali watawajibika kwa Benki kwa muamala wowote uliofanywa kwa kutumia kadi hii kabla ya kupokewa kwa notisi ya maandishi.
32.12 Muda na tarehe ya upokeaji wa notisi ya maandishi utachukuliwa kuwa tarehe ya taarifa kwa Benki.
32.13 Kama ripoti ya hasara au wizi wa kadi hii utatolewa na watu wengine nje ya mmiliki, NMB haitawajibika, kwa hasara yoyote itakayoingiwa na mmiliki wa kadi.
32.14 Wamiliki wa kadi watalazimika kuwa na  uangalizi wa kutosha kuhakikisha usalama wa kadi na usiri wa namba ya siri wakati wote ili kuepusha hasara.
32.15 Wamiliki wa kadi watawajibika kwa madhara yatakayotokana na jukumu  lao linalohusu matumizi na utunzaji wa kadi hii.
32.16 NMB haitajibika na kufichuka siri kwa mtu wa tatu utokanao na matumizi ya ATM au kwa hasara yoyote, uharibifu au madhara yatakayotokana na matumizi ya kadi.
32.17 Wamiliki wa kadi ya pamoja ni lazima wasaini kuonyesha ridhaa yao kwa matumizi ya kadi hii na mmiliki wa kadi aliyeteuliwa na baki ya hesabu kama ilivyotokea kwenye akaunti inayotokana na matumizi hayo.
32.18 Wamiliki wa akaunti ya pamoja ambayo miamala ya kadi imetumwa watawajibika kwa pamoja na mara kwa mara kwa madhara yatakayotokana na jukumu la mmiliki wa kadi kuhusiana na  matumizi na utunzaji wa kadi hii.
32.19 Kadi itakuwa ya halali kisheria mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo kwa uamuzi wa Benki.
32.20 Kadi itabadilishwa kwa uamuzi wa Benki katika tarehe ya kwisha kwa matumizi yake mpaka mmiliki wa kadi atoe maelekezo tofauti.
32.21 Kadi itaendelea kubakia kuwa mali ya NMB na Benki inaweza kusimamisha au kukataa kuhuisha kadi tarehe yake ya kwisha kwa matumizi yake pasipo kutoa sababu yoyote.
32.22 Mmiliki wa kadi hapaswi kabisa kutumia au kujaribu kutumia kadi baada ya taarifa ya ubatilisho au ufutwaji wake kutolewa.  Kadi ni lazima irudishwe Benki.
32.23 Ikiwa mmiliki wa kadi amefariki au amevunja mojawapo ya masharti yaliyo katika mkataba, Benki inaweza kuchukua hatua zilizo muhimu kusimamisha utumiaji wowote wa kadi hii na kufuta matumizi yake.
32.24 Iwapo mmiliki wa kadi hatazuia dhima yake au kutaka maelezo zaidi kuhusu deni kwenye akaunti ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ilipoonyeshwa kwenye taarifa, itachukuliwa kuwa mmiliki wa kadi amekubali dhima/ deni lake kwa Benki.

33 Mkataba kamili
Kanuni na Masharti haya pamoja na Kanuni au Masharti maalumu yanayohusika, mwongozo wa ushuru wa forodha na mkataba wowote mahsusi wa maandishi kati ya Benki na Mteja vinafanya Mkataba kamili kati ya Benki na Mteja.

34 Sheria inayohusika na Mamlaka ya Kisheria
34.1 Kanuni na Masharti haya, Kanuni na Masharti yoyote mahsusi na Mkataba Mahsusi wa maandishi kati ya Benki na Mteja itaongozwa na kutafsiriwa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania.
34.2 Mteja bila kupinga anakubali kwamba Mahakama za  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitakuwa na Mamlaka ya Kisheria katika kuamua kuhusu malalamiko yoyote, tofauti au mgogoro unaoweza kutokea au utakaohusu uhusiano wa Benki na Mteja, ikiwa ni pamoja na Kanuni na Masharti haya, Kanuni na Masharti yoyote mahsusi na mikataba mahsusi katika masharti kati ya Benki na Mteja.
34.3 Bila kuathiri Masharti ya Ibara ya 34.2, Benki itakuwa na haki ya kufungua  mashauri dhidi ya Mteja katika mahakama yoyote nyingine yenye mamlaka halali ya kisheria.

35 Malalamiko
Katika tukio la kusababisha malalamiko, Mteja katika tukio la kwanza atapaswa kumwandikia Meneja wa Tawi la Benki ambako kimsingi Mteja hufanya biashara na iwapo tu Mteja atakuwa hakuridhika ataiandikia Ofisi ya Makao Makuu ya Benki.
 


Nimesoma, Nimeelewa vizuri na nakubali kufuata Kanuni na Masharti ya Hati hii.

 


Mahali:  .................................................   Tarehe: ........................................................

 

 

Jina:  ......................................................                 Saini: ............................................................

 

_______________________________________________________________________________________________________________

Kwa matumizi ya ndani tu:
Imesainiwa mbele ya:


Jina la Ofisa .......................................................................

 


Saini ...................................................................................
_______________________________________________________________________________________________________________

Copyright | Terms and Conditions English| Swahili